Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) limeingia ubia na kampuni ya Power Pool East Africa wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu takribani ya Sh Bilioni 180.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu alisema tayari makubaliano yamesainiwa na serikali NDC kwa niaba ya serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 za hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji binafsi.
Nyalandu alisema kwa mradi huo ambao utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa katika gridi ya taifa na kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadae zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.
“Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo itachukua takribani miezi 15 ili umeme uingie katika gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa” alisema Nyalandu.
Mkurugenzi wa Viwanda vikubwa wa NDC Alley Mwakibolwa alieleza kuwa kwa ujenzi wa mitambo hiyo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme ampema kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ya maji ama ya gesi.
Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadae tutaongeza 50 ili kuoingia katika gridi ya taifa”
No comments:
Post a Comment