Thursday, March 10, 2011

HUDUMA YA BABU YASITISHWAWAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.

Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.

“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda. Habari zaidi

No comments: