Thursday, March 10, 2011

PIKIPIKI AMBULANCE


Serikali imezindua huduma ya pikipiki za kubeba wagonjwa katika maeneo ya vijijini

Akizungumza katika uzinduzi wa matumizi ya pikipiki hizo,Waziri wa Afya Dk Mponda (Pichani) alisema zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya kubebea wagonjwa. Alisema katika awamu ya kwanza, Serikali imenunua pikipiki 400 maalumu kwa ajili ya kubebea wagonjwa zenye thamani ya dola za Marekani 5,900 kila moja.

Waziri huyo alisema pikipiki hizo zitagawiwa katika mikoa yenye matatizo ya usafiri hasa maeneo yenye milima ikiwamo Rukwa, Mbeya, Pwani, Morogoro na Dodoma.

Dk Mponda alisema pikipiki hizo zimekuwa usafiri wa uhakika kwa wagonjwa katika nchi za Afrika ya Kusini, Sudani, Kenya na Senegal, Malawi, Ethiopia na Guinea.

Kama mchina anauza SunLG Sh 1.5millioni angeombwa na kitanda cha pembeni si bei ingekuwa nafuu?

1 comment:

Anonymous said...

ovyo