Monday, March 28, 2011

UVCCM



UVCCM WAACHE KUTAPATAPA


Utagulizi


Kwanza nianze kwa kusema “Ukiona gari (motor car) linapita katika reli (rail way) siyo jambo la ajabu lakini gari moshi (train) likipita barabarani (road way) ni basi ni tatizo kubwa kwani lenyewe gari moshi lina njia yake hiyo tu (specific way) ambapo haliwezi hata kwa dharura kuacha njia yake na kwenda barabarani. Haiwezekani hata siku moja gari moshi liache njia yake ya kawaida halafu bado ionekane n hali ya kawaida


UVCCM ni nini?


Ni jumuiya ya Chama cha mapinduzi iiyoundwa chini ya ibara ya 128(1)(a) ambayo kazi na majukumu yake yameainishwa katika kanuni za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi toleo la 2010; sehemu ya 8 (i-xi)


Kwa mujibu wa sehemu hii ya kanuni za UVCCM hakuna hata moja inayoonyesha kwamba, UVCCM itakuwa na jukumu la kuelekeza nini cha kufanyika na ama Chama Cha Mapinduzi, ama jumuiya nyingine za chama (UWT na Wazazi), ama serikali, ama taasisi ya serikali, ama chama cha siasa ama taasisi ya kiraia, ama mtu yeyote bali pamoja na mengine yote; sehemu ya 8(i) inasema kuwa ni


”kupokea na kutekeleza uhauri; maagizo na maelekezo yote yatakayotolewana Cama Cha Mapiduzi kwa umoja wa Vijna”


Ikiwa Jumuiya imeacha kupokea maelekezo, ushauri n magizo na badala yake yenyewe ndo into maagizo, basi hapa hakuko salama treni imecha reli imeamua kuanza kutembe barbarani, ngoja tuone itafika wapi.


Viongozi wa UVCCM wanajinasibu kwamba wanajivua gamba, ni vema lakini maswali ya msingi wanaloakiwa wawajibu vijana wa Tanzania ni;


i. Gamba wnalojivua na gamba gain na ni nani kawavalisha; au


ii. Ni kwa uzee upi wanajivulia gamba kwani nyoka na mijusi hujivua gamba baada ya kuwa wamezeeka, sasa hawa wanajivua gamba je ni nyoka, na kama wamezeeka kwa nini wasiwaachie vijana wasihitaji kujivua “MAGAMBA”?


Baraza kuu la UVCCM limejinasibu kwa siku za karibuni na kutoa matamko kadhaa pamoja na katibu wake mkuu kuibuka na kumshambulia waziwazi waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa Hal mashauri kuu ya CCM Mh. Frerick Sumaye, si tu ni utovu wa nidhamu bali ni kuacha majukumu na kwenda nje ya wajibu wake kama kiongozi na kama mwanachama wa CCM kwani alichofanya kiko nje ya kanuni za UVCCM, Katiba ya CCM, kanuni za uongozi na maadili (toleo la 2010)


TATIZO LILILOPO


Vijana wengi katika taifa hili wamepoteza imani na jumuiya ya vijana ya CCM. Hii ni jumuiya ya vijana wachache tu waliopo kwenye nafasi za uongozi ngazi ya taifa huko kwingine hakuna matumaini kabisa. Madhumuni halisi ya kuanzisha UVCCM ambayo yanaainishwa katika kanuni zake sehemu ya 7(i-v) yameanza kuachwa tena kwa kasi ya ajabu na hili limewezekana tu baada ya kuingia kwa uongozi huu uliopo na ulichagizwa zaidi baada ya nafasi ya mwenyekiti kukaimiwa na Beno Malisa, huyu kijana ni problem na si tu ni tatizo, bali ameshindwa kabisa kazi aliyoiomba.


UVCCM (hii ya Beno Malisa) inataka lakini kwa maslahi ya wachache kujipambanua kama taasisi pekee ndani ya taasisi kubwa. Kukosa uadilifu, kukiuka kanuni halali za jumuiya na kukiuka katiba ya CCM ni udhihirisho wazi kuwa viongozi wa UVCCM wameamua kuanzisha chama cha siasa ndani ya chama cha siasa. UVCCM inayatambua majukumu yake kama yalivyo sehemu ya 8 (i) ambayo hayajabadilika.


Uongozi wa UVCCM umeshindwa kutekeleza majukumu yake Ikiwa ni pamoja na kushindwa kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ili kukidhi madhumuni ya uundwaji wake katika kupambana na umaskini miongoni mwa vijana. Kwa Mfano kuna chuo cha vijana IHEMI kule Iringa, je wanaweza kusema hata wana lengo lolote la kukifanya hai ili kiwe kitega uchumi cha jumuiya. Tangu wameingia madarakani, ni mradi gain wameubuni ambao una manufaa kwa vijana wa taifa hili? Wameshindwa hata kulima tuta moja la MCHICHA Bonde la Msimbazi, bado wanajinasibu ni viongozi wa jumuiya ya vijana: AIBU


UVCCM inatakiwa kupokea maelekezo, maagizo, ushauri kutoka CCM badala yake yenyewe (UVCCM) sasa imeanza kutoa maelekezo na maagizo kwa CCM, na si kutoa maagizo tu bali wanashinikiza serikali na chama kufanya yale wanayodhani yana faida kwao; hii haiwezi kukubalika ndani ya CCM au serikali.


i. Hivi nguvu ya kumwagiza Rais avunje bodi ya mikopo waliipata wapi?


ii. Nguvu ya kuiagiza SEKRETARIET ya Hal Mashauri kuu ya CCM kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa serikali wanaotoa maoni yao wazi wanapata wapi?


iii. Nguvu kwamba watazunguka nchi nzima kupinga uteuzi w mgombea mabaye si chaguo lao wanaipaa wapi?


iv. Nguvu ya kuiagiza secretariat ya Hal Mashauri kuu ijiuzulu (huku wao hawaonyeshi njia) wanaipata wapi?


v. Wamewataja viongozi wanaodai ni chanzo cha matokeo mabaya kwa CCM 2010 kuwa ni Harison Mwakyembe na Samwel Sitta, na huku wamesahau kwamba wao UVCCM ndio waliozunguka nchi nzima kwa madai ya kuhamasisha na kusahau kuwa Sitta alikuwa Urambo tu na Mwakyembe alikuwa Kyela tu. Hawa Viongozi watuambie; Ni nani aliyewasukumia vijana CHADEMA.


Kwa mwenendo wa tabia, matamshi na utendaji wa jumla, viongozi wa UVCCM wamekiuka kwa pamoja sehemu ya 8 yote ya kanuni za UVCCM, na ibara ya 15(1-8) ya katiba ya CCM inayotaja wajibu wa mwanachama wa CCM. Katika maelekezo ya vifungu hivi vya kanuni na katiba ni ibara ndogo moja tu 15(9) ya katiba ya CCM ndiyo wamefuata ya kuhudhuria vikao vya chama vinavyowahusu; na kama hivi ndivyobasi


Katibu mkuu wa UVCCM pamoja na mjukumu mengine, sehemu ya 87(f) ya kanuni na ibara ya110 (7) ya katiba, zinampa nafasi ya kuwa mjumbe wa Sekretariet ya Hal Mashauri kuu ya CCM.


kwa kuwa basi Baraza kuu katika tamko lake la tarehe 19/2/2011, limeagiza Sekretariet yake yote ijiuzulu kwa kushindwa kumsaidia kazi Rais; na


kwa kuwa Marten Sighela (Katibu mkuu UVCCM) ni mjumbe wa Sekretariet ya chama kwa nafasi yake; na


kwa kuwa katibu mkuu UVCCM amekiri hadharani kuwa ameshindwa kumsaidia kazi Rais (mwongozo wa tamko) na amejipa agizo la kujiuzulu; na


kwa kuwa katika tamko lao hawajaonyesha kama huyu mjumbe kutoka UVCCM amemsaidiakazi Rais kwa kiwango gain;


Basi Shighela aonyeshe njia kwa kuachia ngazi ya ujumbe wa sekretariet ya Hal Mashauri kuu ya CCM, kwa maana hawezi kuendeleea kukaa katika nyumba yeye kwa utashi wake ameona haifai hata kuitwa banda la kuku. Wazungu wanasema “He who know where to go let him show the way” yaani “ajuaye tuendako, aonyeshe njia”


MAADILI


Kuna nadharia kwamba, “Ukitaka kumpiga jiwe mtu aliyeko ndani ya nyumba na humo ndani kuna watu wengine basi lazima ujiandae au ujue yafuatayo yatatokea”;


i. Utafanya uharibifu wa nyumba kwani hakuna namna yoyote jiwe lako litapita bila kuharibu ama madirisha, ama mlango ama chochote.


ii. Jiwe hilo haliampata mlengwa wako kwa uhakika bali litasababishwa mvurugano humo ndani na hata laweza kumkuta mwingine kabisa


iii. Makosa utakayofanya, hayatakuwa tu kumpiga jiwe mtu uliyedhamiria, bali utajumuishiwa uharibifu wa nyumba, mali, samani na kujeruhi watu wengine kadhaa


Hivyo basi, kitendo cha viongozi (Katibu mkuu) kukiuka maadili ya uongozi na badala yake kuanza kuwadhalilisha na kuwatukana viongozi wastaafu (Mfano kwa Sumaye), siyo tu kwamba limemdhalilisha Sumaye, bali;


i. Limeidhalilisha Hal Mashauri kuu y CCM ambayo Sumaye ni mjumbe wake


ii. Limeidhalilisha Kamati kuu ya Hal Mashauri kuu ya CCM ambayo Mzee Sumaye amekuwa mjumbe kwa miaka kumi mfululizo na kutumikia kwa uadilifu


iii. Kwa kudhalilisha taasisi hizi mbili ndani ya Chama (NEC, na KK) basi amekidhalilisha Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake wote.


iv. Amesababisha usumbufu, rabsha na msuguano miongoni mwa viongzi wa chama na serikali kwani Sumaye ni mtu anayeheshimiwa ndani na nje ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Mtu wa aina hii afanywe nini ili hali ndani ya Chama itulie? Sehemu ya 5(2) ya kanuni za uongozi na maadili inaelekeza kwamba ‘kuhakikisha kuwa wanachama wanaovunja maadili ya chama kama yalivyoainishwa katika katiba yaCCM na kanuni za CCM wanachukuliwa hatua za kuwarekebisha na kama itashindikana kuwarekebisha, kuwaondoa katika chama au katika uongozi.


KUOMBA RADHI


Kwa ajili ya taifa na kwa ajili ya faida ya sasa na vizazi vijavyo, ili rekodi zikae sawa isije ikajulikana kwamba taifa hili tangu zamani vijana na wazee hawaheshimiani hata kama wazee wametumika taifa kwa kiasi gain, nachukua nafasi hii mimi binafsi kama kijana wa Tanzania, Mwanchama wa CCM na raia mwema wa Tanzania, kumwomba radhi mzee Sumaye kwa ajili ya;


i. Mimi mwenyewe na vijana wenye mtazmo kama wangu


ii. Vijana wote wa UVCCM wasiokubaliana na maamuzi ya kijinga ya viongozi wao ngazi ya taifa


iii. Watanzania wote walioichukia kauli za Baraza la mkoa Pwani kule Bagamoyo na kauli za baraza kuu kule Dodoma


iv. Chama Cha Mapinduzi ili kisione kwamba vijana wote tumekengeuka, tupo wenye mapenzi mema na Chama hata kama uongozi wa UVCCMunatusukumia CHADEMA


HUSSEIN BASHE


Hivi huyu Bashe ni nani hasa hata akawa na nguvu ya kufanya anayoyafanya?


Iweje Bashe apewe jukumu nzito la kukusanya maoni ya muundo bora wa UVCCM wakati yeye mwenyewe ni tatizo?


Katika kikao chake cha uteuzi wa wagombea ubunge kupitia CCM, Hal Mashauri kuu ya chama ambayo ilitoa tamko kwamba Bashe siyo Raia wa nchi hii, swali la uraia wake bado hajajibu, na hakuna tamko jingine mbadala lililotolewa baada ya hapo, iweje basi mtu ambaye SI RAIA apewe kazi ambayo mustakabali wake una athari kwa vijana RAIA wa taifa hili?


Hivi vijana raia wenye sifa kukusanya hayo maoni hakuna? Huu ndio sasa ufisadi wa hali ya juu kabisa kuingia kwenye kumbukumbu za taifa hili.


Maazimio/Tamko


Ninatoa tamko ambalo litekelezwe ndani ya siku saba kuanzia leo (yaani hadi jumatatu ijayo tarehe 3/4/2011) liwe limetekelezwa;


1. SEKRETARIET YOTE ya UVCCM iitishe press conference kama hii iwaombe radhi watanzania kwa matusi yaliyosababisha chama kudhalilishwa;


2. SEKRETARIET ya UVCCM TAIFA yote iachie ngazi kwani imeshindwa kufanya yale ambayo UVCCM umeundwa kwayo


3. KAMATI YA UTEKELEZAJI yaUVCCM TAIFA yote, nayo iachie ngazi


4. BARAZA KUU la UVCCM lote LIJIVUNJE


Kwa tamko hili, baada ya siku saba kupita UVCCM ibaki katika ngazi ya wilaya tu (ambako vijana wapo) mpaka hapo taarifa mbadala itakapotolewa.


PAUL CHRISTIAN MAKONDA


Mjumbe Wa Mkutano Mkuu Wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini


Mwanachama Wa UVCCM


Simu: 0754754417; 0717213600


makondapaul@gmail.com


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

2 comments:

Anonymous said...

Tuwe na primaries katika ngazi ya urais.

Anonymous said...

JAKAYA KIKWETE AVUNJA SECRETARIETI YA CCM

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amevunja sekretarieti ya chama hicho inayoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, hatua inayoelezwa kufuatiwa na maamuzi mazito zaidi.

Uamuzi huo wa Kikwete umefanyika usiku huu, huku hali ikiendelea kuwa tete mjini Dodoma kunakofanyika vikao vya chama hicho vilivyotanguliwa na sekretarieti na baadae Kamati Kuu.

Kwa mujibu wa habari hizo, Kikwete toka jana ameonekana kuwa mkali na ambaye amekua akitembea na ajenda mkononi huku wasaidizi wake wengine wakiwa hawaelewi undani wa ajenda yake ya mageuzi mazito ndani ya CCM.

‎​Moto ulianza kuwashwa katika kikao cha Kamati Kuu ambako zile tetesi kwamba kuna mkakati wa kumuondoa Kikwete zilipodhihiri kuwa kweli ilipoibuka ndani ya Kamati Kuu hoja ya “kutenganisha kofia za Urais na Uenyekiti”

Taarifa ambazo ziliifikia mtandao wa Jamiiforums.com zilieleza kwamba Kikwete alipoona hoja hiyo imetajwa ndipo alipobaini kuwa “sasa mafisadi wamepania kumng’oa”.

Katika kamati kuu hoja ilikua ni nini kifanyike kuwadhibiti watuhumiwa wa ufisadi na pia kuhusu hatima ya Makamba.

Kwa mujibu wa Jamiiforums.com Kikwete anayo ripoti ya kitaalamu ikielezea sababu za yeye kupata asilimia 60 katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kwamba ilipendekeza kuwa mafisadi watoswe.

Imeelezwa kwamba mjadala wa vikao vya Dodoma utazingatia hotuba ya Kikwete katika sherehe za CCM Februari 5, 2011.

Katika hotuba hiyo Kikwete alisema;

“Hatuwezi kuacha jukumu la kugharamia uendeshaji wa Chama chetu mikononi mwa wafadhili matajiri. Tunahatarisha uhuru wa Chama chetu.

“Chama cha Mapinduzi kiige tabia ya nyoka ya kila baada ya muda fulani hujivua gamba lake na kupata jipya.

“Hatuna budi kufanya hivyo na kufanya hivyo sasa. Wakati wa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa vya tathmini tutalijadili pia suala zima la mageuzi katika Chama.

“Nitapenda tuelewane juu ya namna tutakavyotekeleza agenda hii muhimu kwa uhai na maendeleo ya Chama chetu. Hili ndugu zangu haliepukiki.

“Lazima tukihuishe ili kukiongezea mvuto mbele ya watu. Tuutazame muundo wetu kama unakidhi haja.

“Tuwatazame viongozi watendaji kama wanakidhi haja na kama siyo mzigo unaokipaka matope Chama chetu. Wale tunaoweza kuachana nao sasa tuachane nao kwa maslahi mapana ya Chama chetu.”