Monday, April 03, 2006

25 comments:

Mzee wa Sumo said...

Mzee wa Sumo akiwa na wataalamu wenzake kuitoka Japan kabla ya pambano maridhawa jijini Dar es Salaam hivi katibuni.

Reggy's said...

Mzee wa Sumo karibu sana kwenye blogu. Nimeitembelea na kumuona mwenyewe mzee wa sumo, lakini amevaa tofauti na wenzake wa japan.

John Mwaipopo said...

Mzee wa Sumo tumekuwa tukikusubiri sana katika blogu. Sasa kiu yetu imekatika baada ya wewe kuchukua uamuzi wa papo kwa papo - Lowasa style. Tumiminie mipicha hiyo babu. Tunaitamani ka' nini sijui. Pia blogu yako yaweza kuwa sehemu njema kutunza kazi za picha zako.

Karibu sana mwana kwetu tena usisahau zile picha za kule Mbeya. Najua si haba wewe unazo maana siamini kuwa umesahau kule liliko chimbuko lako.

Jeff Msangi said...

Karibu sana Mpoki.Sumo ya hapa kwenye blogu inakusubiri.Hii ni ile ya kupashana misuli ya habari na burudani.Karibu sana Mpoki

boniphace said...

Wewe Mwaipopo shida yako ni picha za Mbeya tu, una agenda gani ya huko? (Natania hapa) Ok Mpoki furaha hii niliilia siku nyingi. Nashukuru sana kuona mwanga unaowaka hapo Mwananchi The Citizen maana kila siku mtu anaingia hapa. Raha sana ila vipicha tu ndivyo nangoja kwa hamu. Kuna kaujumbe kangu kengine nimekaweka hapo chini kapitie na nadhani utakafanyia kazi mapema.

Mija Shija Sayi said...

'Mzee wa sumo'.. wewe ndiye pawa Bukuku tunayemsikiaga au?

Karibu hadi ndani.

Martha Mtangoo said...

KARIBU SAAAAAAAAAANA Kaka, nafikiri vile ambavyo tulivyovikosa kwa akina Athumani maphoto na kwa Issa Michuzi tutavipata kwako sasa, karibu sana karibu mpaka Chumbani!!!!

Vempin Media Tanzania said...

We Beatrice huoni hatari unamkaribisha huyu jamaa mpaka chumbani shauri yako (natania) Karibu sana muzee wa sumo tulikuwa tukikutarajia lakini ukawa unatu-let down karibu muzee wa sumo ucheze sumo na blogu yako.

Kaka tulitamani sana tukuone ukiwa na kakipago kama wanavyovaa wale wajapani, lakini wewe umevaa suruari tu muzee karibu sana!

Mzee wa Sumo said...

Ahsanteni sana kwa kunikaribisha ingawa bado sijawa na utaalamu wa mablog lakini najua vitu mtapata.

Sitakuwepo kwa wiki moja ama zaidi nataka kwenda Morogoro, Iringa Na Mbeya kuangaliauharibifu wa mazingira, (Si mnajua wazee wa Ari Mpya wamekuja juu), Naenda Usangu, Udzungwa na Ruaha then mambo ntawatumia.

Picha ziko nyingi lakininajaribu kuwa tofauti kwa kuonyesha za hali halisi ya mtanzania kuliko za magazetini ambazo ni za Lowassa na Kikwete. (Karibu watu watawachoka, tunawatumia vibaya).

Peace and Love!

Mzee wa Sumo said...

Mbona kila mtu ana picha kwenye comment, nikitaka kuweka je? Kuna moja nilipiga mwaka 1997 nilipokuwa kijana!

MICHUZI BLOG said...

mzee wa sumo! nimehemewa kwa furaha. unajua, jamaa walikuwa wananipiga mande dunia nzima, kwa vile watu wa snepu tu wachache, yaani sasa kuna mie, wewe na athumani hamisi. ebwana karibu sana. angalia usiwe mvivu kama athumani, la sivyo utajipiga sumo peke yako. naomba utuwekee lile 'kombe' la kunyanyua vyuma uloshinda siku zileeeeee...

Ndesanjo Macha said...

Kweli tuambie mbona umevaa tofauti au sumo ya tanzania ni tofauti?
Hatari...mwananchi na citizen yatakuwa magazeti ya wanablogu. Kuna Omege, kuna Makene, kuna mimi mwenyewe, kuna mzee wa Sumo, kuna Morris, kuna Miruko, na bado....wote hawa familia ya Mwananchi na the Citizen.

Ndesanjo Macha said...

Nilikosea nilitaka kumtaja Kabendera, mmoja wa waandishi wa the Citizen.

Ndesanjo Macha said...

Nikamsahau mwanasafu wa Mwananchi, Yahaya Charahani. Huko Mwananchi na Citizen kumechanjiwa blogu nini?
Moto uendelee.

MICHUZI BLOG said...

shemejio kaniuliza eti nanihii unaiwekaje vile...

ARUPA said...

Mzee wa sumo karibu kwenye ulimwengu wa magazeti tando,hao jamaa wataalamu wenzako sina imani nao maana wanaweza kukuvunja kiuno.

Mzee wa Sumo said...

Wazee nimerudi kutoka Ihefu, sehemu iliyosababisha madhara makubwa kwa nchi kutokana na wafugaji kuvamia bonde la Usangu (Umeme wa Mtera), huko ndio kuna chanzo cha mto Ruaha ama the Great Ruaha ambayo maji hayako katika kiwango cha kawaida. Hali mbaya na inatishia maelfu ya wanyama walioko katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha! Picha zinakuja.

Mzee wa Sumo said...

Wazee nimerudi kutoka Ihefu, sehemu iliyosababisha madhara makubwa kwa nchi kutokana na wafugaji kuvamia bonde la Usangu (Umeme wa Mtera), huko ndio kuna chanzo cha mto Ruaha ama the Great Ruaha ambayo maji hayako katika kiwango cha kawaida. Hali mbaya na inatishia maelfu ya wanyama walioko katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha! Picha zinakuja.

Vempin Media Tanzania said...

Mpoki

acha utani bwana haiwezekani eti kudownload picha kukachukua siku tatu au nne acha utani bwana tunazisubiri hizo picha ni kiasi cha kubandua na kuweka tuletee vituuz.

boniphace said...

Tumechoka kuona picha hiyo tyunajua unazo nyingi au ndiuo umeamua kutubania. Ee bwana mbona unaangusha chama chetu Mwananchi hapo najua wewe unataka niseme Citizen haya mbona unaangusha chama?

Indya Nkya said...

Karibu Mzee wa Sumo. Tupo wote

mloyi said...

Labda alitaka tuone jinsi anavyotisha na hayo mavazi ya kiuchiuchi,

Rashid Mkwinda said...

Unajua mi nilishangaa kuona mzee wa Sumo akikabiliwa na wajelajela eti kwa sababu ya kupiga picha kule Ukonga ningekuwa mimi ningewaaaaapa zile za kichinachina, kuna haja ya waandishi kupitia katika mahekalu ya kujilinda.(jokes)

Au inawezekana ile adha ya wajelajela pale Ukonga ikakusukuma kujiunga na Wana sumo ili siku nyingine wasithubutu kufanya mchezo wa aina ile?

Mie bwana nisingekubali kingeeleweka mbele ya safari lakini lazima na wao ningewapa ngeu kwa nini watuchezee namna ile.

Juzi nilikuwa naperuzi habari inayohusu ile kesi ya wajelajela na Mzee wa Sumo nilimnukuu akisema kuwa akiwaona wajelajela anajisikia kichefuchefu, mimi nadhani, hawa wajelajela nnndio walitakiwa wakituona sisi wajihisi kutapika baada ya kuwateremshia kisago.

Lakini pamoja na yote yaliyojiri Mzee wa Sumo karibu kilingeni kama alivyosema Ndesanjo naona wadau wa Mwananchi Communication wamechanjia Blogu.

Karibu sana kijiwe huru hakuna wajelajela wala akina Mapuri huku ni fikra zako na mchango wako wa busara ndio unaotakiwa.

Mzee wa Sumo said...

-Jamani nimerejea tena ulingoni baada ya kufariki kwa muda mrefu!

Rundugai said...

Haya saasa Mwananchi mnatisha naona kuna jamaa wanawanyemelea Tanzania Daima kwa blogu hii inatia moyo tuwe wengi mpaka tutishe tuumize vichwa>Mzee wa sumo unatisha hii sumo yako ya Suruali ni ya wapi hii PICHA ZIje kwa wingi