Saturday, January 19, 2008

UTENZI

Jamani kuna mdau katuma utenzi huu sijui Muunguja?

Utajulikana ukweli,
Mafisadi kuwakabili,
Na kuwapiga kabali!

Tutawaumbua wazi,
Na walie kama mbuzi,
Ufisadi siyo kazi,
Ya kujifanya wajuzi!

Fisadi numero uno,
Yule mwenye majivuno,
Kajijazia mavuno,
Na pesa kama unono.

Jina lake ni Mkapa,
Aliyetutoa kapa,
Katuacha tunakopa,
Na sasa anatuepa.

mwingine ni Balali,
Huko aliko halali,
Kakimbilia mbali,
Ataletwa na madalali .

Anayefuata Mramba,
Ni yule aliyetamba,
Kumbe kinara wa pumba,
Na fisadi mwenye namba.

Kasema tule majani,
Ni kejeli ya kihuni,
Pateli na kina nani,
Kawakumbata kundini!

Mwingine ndiye Mgonja,
Hazina kawa kiranja,
Akala njama kijanja,
Cha moto atakionja,

Kikwete yu matatani,
Hajui afanye nini,
Mkapa afanywe nini,
Mtama wasimwageni?

Alisema muacheni,
Kastaafu jamani,
Wazee waheshimuni,
Mwawabughudhi ya nini?

Njia panda amekwama,
Zilipenya kwenye chama,
Benki Kuu walichuma,
Madongo yamewakwama!

Sitaki kuenda sana,
Kaditamati na tana,
Fisadi mnawaona,
Wako kimya wametuna!

No comments: