Saturday, May 31, 2008
TAIFA STARS LEO
Stars 1-Mauritius 1
Ilikuwa patashika Uwanja wa Taifa leo lakini mashambulizi yetu yote hayakuzaa matunda. Tumepata nafasi zaidi ya 15 na kona kama 26 lakini tumetoka patupu!
Pamoj ana udhanmini wa nguvu lakini bado Stars haijakaa sawa, mpira ulikuwa bomba lakini magoli haba.
Danny Mrwanda ndio aliyeokoa katika kipindi ch apili baada ya watanzania kuchanganyikiwa kwani Mauritius ilikuw ainaongoza 1-0 hadi kipindi cha kwanza kinaisha.
Lakini pamoja na hayo watanzania wamegundua tatizo sio kocha bali ni washambuliaji ndio hawajaiva, sijui iweje maan awaliopigiwa kelele wawekwe ndio wameshindwa kufanya mambo! Maximo huyooo anatimua baada ya mechi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Mi naomwachezaji wa nje warudishwe kuipa nguvu stars. Jamani naomba muelewe kucheza nje ni kucheza nje hata kama unacheza barabarani. renatus njohole ana uwezo mkubwa wa kumiliki hicho kiuongo sio huyo tu mimi nawajua wachezaji kibao wenye uwezo wa kuisaidia stars lakini wako wanaga gaa tu. wapeni nafasi hawa!
kwa kweli maximo asilaumiwe naungana na mzee wa sumo,hata hivyo vijana walionyesha kuchangamka zaidi kuliko mechi walizowahi kucheza awali. waosha vinywa waendelee tu kuchonga kwanza wengi wao hawakuona mpira ulivyokuwa zaidi ya kupata habari bloguni.
kila staa wa kibongo ameshachaguliwa kuichezea timu ya taifa lakini matokeo ndio haya tunayoyapata..Machupa, Mgosi,Abuu Ramadhani, Kaniki na sasa Gabriel, wote hawa wameshaichezea timu ya taifa lakini hakuna significant changes!!..tatizo sio kocha , tatizo ni kwamba hawa wachezaji hawakuandaliwa kitaalam wakati wangali wadogo..Tanzania tulikuwa tunapiga sana siasa..tulikuwa tunahangaishana na akina Ndolanga wakati wenzetu kina Senegal, Cameroon, Zambia ,Tunisia , kwa kutaja wachache, wakiandaa timu zao za vijana..wenzetu wamegharamika sana kuweza kutengeneza timu imara za Taifa walizonazo kwa sasa..wabongo tunapaswa kuwa wavumilivu kama tunataka kuona maendeleo ya kweli ya soka
Post a Comment