Rais Jakaya Kikwete, ameteua majaji 11 wapya kati yao saba ni wanawake.
Taarifa ya Ikulu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, ilisema kuwa uteuzi huo umeanza Jumamosi, Mei 24, 2008.
Walioteuliwa kuwa majaji ni Sophia Wambura, Crecencia William Makuru, Zainabu Goronya Muruke na Upendo Hillary Msuya.
Wengine ni Atuganile Florida Ngwala, Rose Aggrey Teemba na Rehema Kiwanga Mkuye.
Majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Kassim M. Nyangarika, Gabriel Kamugisa Rwakibarila, Ibrahim Sayida Mipawa na Lawrence Kisenge Nziajose Kaduri.
Katibu Mkuu Kiongozi ametangaza pia kwamba, Rais Kikwete amemteua Ferdinand Leons Katipwa Wambali, kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Bwana Wambali anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Sophia Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.
Kabla ya uteuzi wake, Wambali alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani.
Rais amefanya uteuzi huo pia ikiwa ni takriban mwaka mmoja sasa tangu ateue majaji wengine 20, ambao alifanya baada ya bunge la bajeti la mwaka jana.

No comments:
Post a Comment