Wednesday, May 28, 2008

ZOMBE


Kesi ya Zombe inaendelea kuunguruma mahakamani na watu wamekuwa wanatoa ushahidi, inaonyesha kuwa na mvuto, sijui wadau mngependa kuwe na updates kila siku? Nawasikiliza na sasa hivi nataka kazi iwe moja kwa moja. Vilevile ningependa kujua watu wanainterest na vitu gani ili nijue vitu vya kuweka katika blog hii!

7 comments:

Anonymous said...

hii kesi ni tamu sana kuisikiliza ni kama movie fulani hivi iliwahi kutokea pale Bongo. ni vema tukapeana updates il tuone mwisho wake. yawezekana sheria ikapindwa hivihivi na Tz ilivyojaa mafisadi.

Anonymous said...

Mkuu, interest yangu kubwa ni kuona updates za mambo mbalimbali, haijalishi ya nini.. ila mradi tu nione habari mpya katika blog yako walau kila siku.
Ze mdau

Anonymous said...

Mzee wa Sumo,

Kwa sisi tulio ughaibuni basi tungeomba uwe unatupa updates za hii kesi ambayo inagusa hisia za watu wengi unajua ni nadra mambo kama haya kutokea pale watu waliokuwa na madaraka ya kusema ua watu wakaua kuwaona wanapandishwa kizimbani. Hii inatoa fundisho la kuona namna gani haki inatendeka.Endelea kutupasha.

Anonymous said...

yaa tunahitaji updates za Zombe na kesi yake kila siku hadi iishe. Unajua swala lake lina maslahi sana kwa wananchi.
Asante na kazi njema

Anonymous said...

mwenendo kuhusu kesi ya zombe ni muhimu sana kwa sasa kuuripoti kila inapotajwa inagusa hisia za jamii kubwa kwa sasa.

Anonymous said...

muheshimiwa yaani ikiwezekana hata kuturekodia itakuwa poa zaidi maana hawa jamaa na mkuu wao zombe walifanya ishu hii kwa makusudi mimi nilizipata nikiwa bongo kwa mshikaji wangu ambaye ni askri maarufu hapo bongo kuwa ishu hiyo ni zombe mwenyewe aliye amuru kuwa peleka pwani kwa ajiri ya kuchukua huo mshiko. tupe up to date mzee.

Anonymous said...

Mzee wa sumo, naomba uwe unaweka mahojiano kama ulivyoweka hapo juu. Kama unaweza kwenda na tape recorder (kama inaruhusiwa) then itakuwa safi kama utatuwekea hapa mahojiano.

Mdau wa US tawi # 1