Friday, June 13, 2008

Mwakyembe augua ghafla bungeni!!


MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ameugua ghafla akiwa bungeni na kukimbizwa hospitali.

Dk Mwakyembe ambaye aliongoza Kamati ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa
Ushindi wa Kuzalisha Umeme wa Dharura kwa Kampuni ya Richmond Development,
aliingia bungeni jana akiwa na afya njema, lakini hali ilibadilika ghafla na kutaka kuanguka.

Aliingia bungeni majira ya saa 2:00 asubuhi akiwa na afya njema, lakini ilipotimu saa 3:30 asubuhi alianza kujisikia vibaya, huku akitaka kudondoka chini.

Hata hivyo, Mbunge wa Lupa(CCM), Victor Mwambalaswa alibaini hali hiyo na
kumuondoa bungeni pole pole akiwa amemshikilia na kumtoa nje ya Ukumbi wa
Bunge.

Baada ya kumfikisha nje, Mwambalaswa aliita gari la kubeba wagonjwa na
kumkimbiza kwenye kliniki iliyopo majengo ya Bunge ambako alipata huduma
ya kwanza, lakini baadaye alihamishiwa sehemu ambako haijulikani.

1 comment:

Anonymous said...

unajua wabunge wengi vimeo ni bora wakaangaliwa afya zao kabla ya kupitishwa kuwania ubunge hata hivyo pole sana babake