Tuesday, July 01, 2008

WATOTO WA AJABU

WATOTO wawili wenye maumbile yasiyokuwa ya kawaida wamezaliwa kwa nyakati tofauti katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa .
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Iringa, Dk Oscar Gabone alifahamisha kuwa mama mmoja mwenye umri wa miaka (45) amejifungua mtoto wa ajabu asiye na kichwa.

Dk. Gabone alisema mama huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji na mtoto wake aliyekuwa na jinsia ya kike akiwa hana kichwa, lakini alifariki akiwa tumboni.

Katika tukio jingine, mwanamke mwingine mkazi wa Iringa, mwenye umri wa miaka (30) alijifungua mtoto mwenye kitovu kilichovilingishwa vitu vinavyofanana na kamba.

Kwa mujibu wa Dk Gabone kichanga hicho chenye jinsia ya kiume kilifariki dunia masaa matatu baasa kuzaliwa na kwamba huyo alikuwa mtoto wa kwanza wa mama huyo.

2 comments:

Anonymous said...

mpoki tafuta mapicha basi tuone.inasikitisha kwa kweli.

Anonymous said...

MIAKA 45 ANAZAA? mmmh!