Tuesday, August 26, 2008

AJALI BONGO

Basi la kampuni ya Kimambo Express likiwa limepinduka baada ya ajali na gari dogo (chini) katika eneo la Nane Nane mkoani Morogoro na watu wawili kupoteza maisha.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo ya Morogoro.
Lakini wakati watanzania wenzetu wanapoteza maisha na kupata vilema vya kudumu ni nini kifanyike ili kuepuka na ajali kama hizi ambazo kila siku zinatokea? Hili ni tatizo la umaskini ama uzembe?

5 comments:

Anonymous said...

hili sio tatizo la umaskini hili ni tatizo la uzembe na ujuha.rushwa,ya polisi wa barabarani,rushwa wanaopewa wale wanaopasisha magari na kutoa leseni za madereva kiholela ,hao wanabidi kuwajibika na kuelimishwa na kukumbushwa wajibu wao mara kwa mara.pia sheria za barabarani ziwe zinafuatiliwa bila kumuogopa dereva au wadhifa wa dereva anapofanya kosa au uzembe.inabidi kupigwa faini na kifungo cha jela kwa muda mrefu.na kunyang'anywa leseni yake

Anonymous said...

Kamwe sio umaskini wala uzembe. Hii ni LAANA. "Kweli nchi ya kitu kidogo ni nchi ya watu wadogo" Rushwa na kutofata sheria za nchi vimetufikisha hapa tulipo. Tunahitaji nguvu za pamoja kuyapinga haya

Anonymous said...

RUSHWA ni adui wa haki-J. K. Nyerere.

kauli hiyo ni nzito sana. Ajali hizi chanzo kikubwa ni rushwa ndio mengineyo yanafuata. Magari mabovu mengi tu yako barabarani kwasababu ya rushwa, madereva wasio na staha za udereva wapo barabarani kwa sababu ya rushwa. Inafaa ifahamike kuwa udereva wa abiria ni weledi kama ulivyo urubani au unahodha au udereva wa gari moshi. Hivyo maadili yake yazingatiwe kwa umakini mkubwa ikiwemo mafunzo thabiti, umakini katika utoaji leseni, uhakiki wa stadi na nidhamu za madereva mara kwa mara, na adhabu kali kwa wote watakaobainika kusababisha ajali na upotevu wa maisha na mali.

Vile vile watanzania tusimame imara sasa tusipelekwe kama mang'ombe,tuachane na dhana za kutegemea serikali itufanyie hili na lile kuna mambo mengine yako ndani ya uwezo wetu likiwamo kuwakanya madereva wenye mienendo mibovu wakati wawapo kazini, kama kunywa pombe, kutokuwa makini, nk. Tusipoamka nakuitegemea serikali tu tutakwisha inabidi sisi ndio tuiamshe serikali kuwa wananchi tupo na tuna nguvu. AMKA Mtanzania AMKA....!!!!

Anonymous said...

kwa kweli huu ni unyama kwani hao mapolisi wanapopokea rushwa ili kutoa leseni kwa watu wasio na uwezo ni kwa sababu gani????????? sasa basi serikali na iangalie upya suala hili la ajali barabarani zinavyoteketeza familia na kupunguza koo za watu, iandae mpango wa kukagua leseni na pia uendeshaji wa madereva wanaopewa leseni na wajomba zao au kwa njia ya rushwa. KWA KWELI NI MASIKITIKO MAKUBWA SANA KWA HIZI AJALI ZA BARABARANI ZINAZOHUSISHWA NA MABASI YA ABIRIA. MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN. NA NDUGU ZETU WALIOUMIA MUNGU ATAWAPA AFUENI MAPEMA. Kabby

Anonymous said...

Pamoja na Yote mazuri katika blog yako... tafadhali jaribu kuchuja PICHA hapa hukuweka age limits hivyo yeyote anaweza kuangalia hata watotot ...
hii picha ya mwisho huyu mtu aliyefungwa mabendeji haikustahili kuonyeshwa hapa kwani X sio picha za utupu tu! hata za namna hii nazo si za kuweka ktk blog ambayo ni huku kwa umri wowote .....