Wednesday, August 06, 2008

DAWASCO VIPI?

Mdau kaniuliza hivi:Mpoki naomba ufuatilie tatizo la Dawasco Kibamba eneo la kwa mangi mji mpya,ambao tuko chini ya Dawasco Kibaha, kuna vishoka wanakata mabomba au ni wafanyakazi wa Dawasco wanakata mabomba ukienda kufuatilia ofisini kwao tatizo ni nini? Unaambiwa umeconnect kwenye bomba la inch 30 badala ya inch 24, ninachouliza we ukienda kuomba uunganishiwe maji wanakuja kufanya survey then wanakupa gharama ukilipia wanakuunganishia, hao hao wanadai umeunganusha kimakosa unakaa bila maji, utandaji wao wa kazi siuelewi wanaendekeza Rushwa kila kitu ili kiende haraka lazima uwaachie kidogo dogo, hii nci haki iko wapi na bado umeunganisha kihalali wanakunyanyasa, viongozi wa Dawasco mko wapi? Mnakosa hela za kihalali kwa sababu ya wapuuzi wachache wanahujumu miundo mbinu, Inakera sana. Mdau

No comments: