Tuesday, August 05, 2008

FAMILIA YA CHACHA YAJA JUU!

Kaka wa Marehemu Cahacha, Profrsa Samweli wangwe akizungunza na waandishi
Kifo cha Wangwe chageuka


WAKATI familia ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ikihoji maswali tisa yanayomhusu Deus Mallya, ambaye alikuwa na marehemu wakati ajali iliyoondoa maisha yake, kundi la vijana wanne wanaodai kusafiri na Mallya kwenda Libya limeibuka na kumtetea kijana huyo kuwa hahusiki na vitendo vya kijasusi kama baadhi ya wakuu wa vyama vya upinzani wanavyodai.
Akitoa tamko la familia, jijini Dar es Salaam jana, kaka wa marehemu, Prof Samuel Wangwe, alisema bado chanzo cha ajali hiyo kina utata na kutaka maswali tisa yanayomhusu Mallya yajibiwe.
Profesa Wangwe alisema, bado kuna utata kama ajali hiyo ni ya kawaida au kupangwa, na kama ilipangwa basi ilipangwa na nani?
Katika msimamo huo alioutoa mbele ya wahariri wa vyombo vya habari na alisema: "Kuna utata mkubwa kama ajali iliyopasaua kichwa cha ndugu yetu ilitokea pale katika eneo la ajali au kabla. Familia imekuwa shaka na chanzo cha ajali kutokana na taarifa mbalimbali zinazopingana hasa zinazotolewa na Mallya na baadhi ya wananchi waliofika katika eneo la ajali na mazingira mazima yanayohusu uhusiano kati ya Deus Mallya na ndugu yetu Chacha."
Profesa Wangwe aliyataja maswali ambayo familia inahitaji uchunguzi wa kina ufanywe kuwa ni
Moja:Kwa nini Mallya alianza urafiki na marehemu hivi karibuni ndani ya wiki tatu au nne na urafiki huo ukawa wa karibu kwa haraka namana hiyo na kwamba ulikuwa unashinikizwa na nani?
Pili:Ni kwa nini Mallya alikuwa anashinikiza safari hiyo ya usiku wakati watoto wa Wangwe na mke wake walishauri asisafiri siku hiyo usiku;
Tatu: Ilikuwaje Mallya aonekane ana shida na safari hiyo kuliko watu wengine wakiwemo marehemu mwenyewe watoto na mkewe.
Nne: Familia hiyo inataka kujua kwa nini awali Mallya hakutaka ajulikane kwamba ndiye alikuwa akiendesha gari.
Tano: Kwa nini hajaeleza kuhusu mtu wa tatu aliyeonekana kuwa pamoja naye kwenye tukio la ajali.
Sita: Familia inataka ufafanuzi wa mtu wa tatu aliyetoweka baada ya kuonekana na waliofika katika eneo la ajali alikuwa anakimbia nini.
Saba: Inataka kujua kwa nini laptop ya Mallya ambayo alikuwa akifanyia kazi zake nyingi, ilitoweka baada ya ajali wakati simu na fedha zilikutwa eneo la ajali. Katika swali la saba familia inataka kujua kama ni kawaida kwa wananchi wa kawaida kuchukua laptop kuliko kuchukua simu na fedha.
Nane: Wanataka kujua kwa nini Mallya alidai ameondoka Dodoma saa 9 mchana wakati familia yake inajua kwamba waliondoka baada ya saa 12 jioni.
Tisa: Wanafamilia hao wanataka kujua kwa nini Mallya hakutaka ifahamike kwamba waliondoka usiku.

No comments: