Tuesday, August 12, 2008

KIKOSI KINGINE STARS

KIWANGO kilichoonyeshwa na chipukizi, Jabir Azziz, Adam Kingwande, Amani Simba na mkongwe Mussa Hassan 'Mgosi' -wote kutoka Simba- kimetosha kumfanya kocha Marcio Maximo kuwaita wachezaji hao kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Lakini, Mbrazili huyo amemuacha mshambuliaji Emmanuel Gabriel, viungo Ulimboka Mwakingwe na Abdi Kassim, ambao hawakung'ara kwenye mashindano hayo ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, pamoja na kipa ambaye bado hajajaribiwa, Shaaban Dihile wa JKT Ruvu.
"Siku zote huwa naangalia uwezo wa mchezaji na wala sio jina," alisema Maximo wakati akitangaza kikosi jana.
"Nafurahi sana ninapoona timu zetu, hasa Simba na Yanga zikiwa na wachezaji vijana. Nafikiri haya ni maendeleo makubwa ya soka kwenye nchi hii."
Mgossi, ambaye aliachwa kwenye kikosi cha Stars mapema mwaka jana, aliibuka kuwa mfungaji bora wa Kombe la Kagame mwezi uliopita, wakati Kingwande, Jabir na Amani, ambao ni wapya Stars, waling'ara wakati Simba iliposisimua mashabiki kwenye michuano hiyo kabla ya kuangushwa na URA ya Uganda katika nusu fainali.
Stars itaingia kambini kesho kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ghana, Black Stars itakayofanyika jijini Dar es salaam Agosti 20 na baadaye kwa mechi mbili za michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan, kabla ya kukabiliana na Cape Verde na Mauritius katika mechi za Kombe la Dunia/Mataifa ya Afrika.
Katika kikosi kilichotangazwa jana na Mbrazili huyo kuna sura nyingi zilizokuwepo kwenye kikosi kilichosisimua mashabiki baada ya kuipa wakati mgumu Cameroon katika mechi mbili za Kombe la Dunia/Mataifa ya Afrika.
Lakini, pia ameita wachezaji watano chipukizi ambao wataingia kwenye programu kama iliyowakomaza Jerry Tegete na Kigi Makasi, kwa ajili ya kujifunza.
Kikosi kamili:
Makipa- Ivo Mapunda (Yanga), Aman Simba (Simba). Farouk Ramadhan (Miembeni).

No comments: