Saturday, December 27, 2008

JAMANI MJIHADHARI


Mshikaji amekamatwa akiwatoa upepo wananchi akijifanya polisi, hii imekuwa noma sasa sijui nani aaminiwe? Ama ndio inatakiwa ukikamatwa ung'ang'anie kwenda kituoni? Jamaa aliingia mkenge akamkamata polisi zikawa arobaini zake. Take care ndugu zanguni!

5 comments:

Anonymous said...

Hii ni kali maana akili kichwani. Hakuna mtu anayetaka kulala njaa.

Anonymous said...

jamaa kawa mpole kinoma,infurahisha kweli, lakini inatisha sana.
ndo tanzania tunayoijenga ,akili mkichwa.

Mzee wa Changamoto said...

Natumai wataanzia uchunguzi kwa alikozipata hizo sare.

Anonymous said...

basi huyo hata dhamana hatapewa utafikiri kafanya mkosa mkubwaaaaaaaaaaaaaaa kuliko wale waheshimiwa waliolitia hasara taifa la mabilioni kina mramba na yona,lowassa,chenge nk akipelekwa kwa hakimu huyo hakimu anaweza akakurupuka tu 20yrs kumbe kuna wakubwa waliosababisha jamaa afanye hivyo kwa ukata

Anonymous said...

Huyo jamaa dingi yake au kaka yake anaweza kuwa polisi akampa magwanda hayo akipigie deiwaka... au mwenyewe aliyakwapua kwa ndugu yake akapige deiwaka kama madereva wa daladala wavyowaachia makonda magari wakapigia deiwak...