Saturday, December 27, 2008

NKURUZINZA NA WAREMBO MISS EA

Rais Pierre Nkurunzinza akiwa na Miss East Africa, Claudia
Niyonzima, mshindi wa tatu, Rahwa Ghebrehiwet na mshindi wa pili, AnneteMwakaguo ambaye anatoka Tanzania

Rais Nkurunzinza akiwa na Mkurungenzi wa Rena Events, Rena Callist
(kushoto), Miss East Africa, Claudio Niyonzima (KULIA). Wengine kutokakushoto ni Serge Nkurunzinza, Annete Mwakaguo wa Tanzania ambaye nimshindi wa pili na Rahwa Ghebrehiwet wa Eritrea ambaye ni mshindi wa tatu.


RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza awaomba waandaji wa mashindano ya Miss East Africa kuyarudisha tena nchini Burundi hapo mwakani.
Akizungumza katika hafla aliyoiandaa Ikulu mjini Bujumbura jana, RaisNkurunzinza alisema serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa kwa waandaji ambao ni kampuni Rena Events Limited ya Dar e salaam, Tanzania.
Alisema mashindano ya mwaka huu yaliyomalizika wiki iliyopita yalifanyika kwa mafanikio makubwa na amewapongeza waandaaji kwa kuyaandaa mashindano
hayo kwa kiwango cha juu na kutangaza utamaduni na utalii wa nchi ya Burundi kwa kiasi kikubwa.
Rais Nkurunziza alikutana na Mkurugenzi wa Rena Events, Rena Callist, Miss East Africa 2008, Claudia Niyonzima, mshindi wa pili, Anette Mwakaguo wa Tanzania na mshindi wa tatu Rahwa Ghebrehiwet na mratibu wa Miss East
Africa nchini Burundi, Serge Nkurunzinza.
Rais pia alimpongeza mrembo Claudia ambaye anatoka Burundi kwa kushinda taji la Miss East Africa 2008.
Kwa upande wake Callist aliishukuru serikali ya Burundi kwa kuwezesha mashindano ya Miss East Africa 2008 kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Naye Miss East Africa 2008, Claudia alimweleza Rais Nkurunziza kwamba baada ya kushinda taji hilo, sasa ana wajibu mkubwa wa kutimiza lengo la mashindano hayo kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ki jamii, na
kwamba kwa mwaka huu lengo la mashindano hayo ni kusaidia watoto yatima na kuahidi kwamba atatimiza malengo yaliyokusudiwa.
Miss East Africa imeandaa bahati nasibu itakayo chezeshwa katika nchi tano kuanzia mwezi ujao ili kusaidia watoto yatima, ambapo Rais Nkurunziza ameahidi kusaidia bahati nasibu hiyo na kuwaomba watu wote wa Afrika ya
Mashariki kuunga mkono bahati nasibu hiyo.

No comments: