Thursday, January 22, 2009

AJALI
WATU 15 wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa vibaya baada ya magari matano kupata ajali katika daraja la mto Nduruma, wilayani Arumeru, Arusha jana mchana.
Katika tukio hilo, basi dogo lililokuwa na abiria lilitumbukia katika mto huo na kusabaisha vifo na wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya mkoa wa Arusha, Fransis Coasta, hadi jana jioni, miili sita kati watu 15 walikufa katika ajali hiyo ilikuwa imetambuliwa.
Miili hiyo ni ya askari wawili wa upelelezi ambao walikuwa wamepeleka mtuhumiwa mkoani Kilimanjaro, CID Hamidu na CID Abiel.
Wengine ni Mtawa, Anastazia, Mchungaji Peter Maina, David Ngunda na Alice Kinga wote wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Majeruhi ambao hadi jana walikuwa wamelazwa katika hospitali hiyo ni Josepheni Boniface, Scolactica Samson na Maria Apolonary.
Wengine ni Exaud Mbide dereva wa gari Land Rover, Deogratus Gabriel. Leka Chuwa, Sebastian Tarimo na Ailali Damian.
Majeruhi wengine ni Sloyce Joachim, Elia Abdalah, Dismas Patrece na Isack Angalili ambao wote bado hali zao sio nzuri na baadhi walitarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Ajali hiyo ambayo ilisababishwa kufungwa kwa barabara ya Arusha, Moshi kuanzia mchana hadi saa 12 jioni ilitokea baada na magari hayo kukutana katika daraja hilo jembamba na kugongana.


No comments: