Wednesday, February 11, 2009

MWENYEKITI WA IPP ANAPAKAZIWA


Picha za Mengi zinazodaiwa kupigwa baada yakufunga ndoa na huyu mrembo!

Mengi akizungumza na waandishi jana kukanusha mambo mbalimbali pamoja na ndoa hiyo.
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi jana alikanusha taarifa ya gazeti moja kuwa amefunga ndoa mpya na mwanamke wa jijini Dar es salaam na kulaumu uandishi wa habari unaokiuka misingi ya kitaaluma.

Mengi aliripotiwa na gazeti hilo la kila wiki kuwa amefunga ndoa nyingine, huku gazeti hilo likichapisha picha zinazomuonyesha mfanyabiashara huyo maarufu akiwa na mwanamke huyo.

Mengi, ambaye ni Mkristo, anadaiwa na gazeti hilo kuwa alifunga ndoa hiyo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mengi alisema kuwa hajawahi kufunga ndoa nyingine akisema taarifa hizo ni uongo mtupu.

Badala yake, Mengi alizihusisha taarifa hizo na mikakati ya mafisadi ambao alidai wanamchukia kwa sababu yuko mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi.

Mengi aligeukia uandishi wa habari na kusema kuwa umeibuka 'uandishi wa kuchafuana' katika baadhi ya magazeti ya wiki, akisema hiyo inatokana na baadhi ya watu aliowaita mafisadi.

Alisema mafisadi kwa kutumia baadhi ya magazeti hayo ambayo wameanzisha au kuyafadhili na wamekuwa wakipotosha ukweli wa vita dhidi ya ufisadi huku baadhi ya waandishi wakiingilia faragha za watu.

"Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Baraza la Habari Tanzania (MCT) linatakiwa kutoa msimamo wake juu uandishi wa mambo ya faragha," alisema Mengi katika mkutano huo mfupi.

"Fitna na uongo unaosambazwa na mafisadi hawa ni sumu, inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani."


No comments: