Wednesday, February 11, 2009

MILIMANI

Mwanzoni niliona rahisi nikawanapumzka bil aya taabu!
Watu wakaendelea kukwea tu wakitafuta kilele kinaitwa Lenana.

Wakakiona kilele wakaendelea na safari ya kukifikia!
Kufika Kileleni huyu Singasinga wa Kikenya (mkorino) akaweka bendera ya Nation pale juu, safari ikawa ndio hiyo!
Kilele chenyewe hiki yaani vifo vingine tunavyovuitafuta!
Cheki watu walivyokuwa hoi kupanda mlima, sura kama naniii..
Kumbe snow inashikika hata kwenye tropiki?
Hapa tunakaribia kilele ingawa mshikaji wangu kulia alikuwa amekata tamaa kabisa, akarudi!
Dezaini hii hapa nikuwa hoi kumbe kadri unapokwenda juu mapafu yanafunga? Sasa mavazi kama haya watoto wakikuona si wanakimbia?


Jamani watu wengine kwa kubonda, eti wakasema kuwa sijui kuupload ndio maana sijaonekana kwa muda! Hivi tu ukiwa milimani namna hii kunakuwaga na network? labda mlima Everest ambao sijawahi kupanda! Acheni kuua, Nilikuwa mlima Kenya kwa jili ya kuchangia binadamu wanaokabiliwa na njaaa, hamtaki niende peponi kwa vijisifa vidogovidogo? Watu wanasema eti mzee wa Sumo bonge nyanya, cheki nilivyofiti!1 comment:

EDWIN NDAKI said...

Karibu mzee wa Sumo..

maana sasa najua gurudumu litasukumwa kama kawa...

nimecheka sana haka kamstari kwenye picha zako.."hamtaki niende peponi kwa vijisifa vidogovidogo? "

kazi nzuri sana kuwakumbuka wenye shida..pamoja mpoki