Saturday, March 07, 2009

ZA MWIZI 40!!!

Mtu anyedaiwa kuwa mwizi akiwa ndani ya boksi baada ya kuhifadhiwa na wenzake katika duka la jumla kama mzigo maeneo ya Mwanjelwa mjini Mbeya kwa lengo la kuiba fedha katika duka hilo hivi karibuni. Lakini bahati haikuwa yake kwani mmiliki wa duka alishtuka na kuwataka walioleta boksi kulifungua nao kukataa na kutimua mbio. Baadae alipolifungua alimkuta mtu huyo na kuamua kupiga mayowe ya msaada ndio wananchi walipofika na kumshughulikia akiwa andani ya boksi hilo.


1 comment:

Anonymous said...

hii kali nayo sasa ona walivyomsulubisha.