Tuesday, April 21, 2009

SENDEKA MATATANI


KESI inayomkabili Mbunge wa jJimbo la Simanjiro, Christopha Ole Sendeka jana ilichukuwa sura mpya baada ya upande wa mashitaka kumuongezea shitaka jingine la kumtishia kumpiga kwa bastola Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapindizi (CCM) mkoa wa Arusha, James Ole Millya.
Licha ya kusomewa shitaka hilo la silaha, pia upande wa mashitaka jana ulieleza mahakama kuwa wanatarajia kuwaita jumla ya mashahidi 13, akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Vicent Kone ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Simanjiro na viongozi wengine wa CCM.
Mwendesha mashitaka wa Serikali, Michael Luena alisema shitaka la kwanza linalomkabili Sendeka, ni shambulio ambalo anatuhumiwa kumpiga Ngumi na kibao Millya Januari 9, mwaka huu wilayani Monduli na kumsababishia majereha.


No comments: