Tuesday, May 12, 2009

ROSTAM VS KUBENEA



Leo jijini Dar es Salaam Rostam Aziz ameweza kushinda kesi ya madai ya fidia baada yakuandikwa 'vibaya' na gazeti la Mwanahalisi. Mahakama imeamuru alipwe fidia ya Sh3bilioni kwa kuwa Mwanahalisi wameshindwa kuthibitisha ukweli wa story mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na gazeti hilo.
Rostam ambaye ni Mbunge wa Igunga alidaiwa kuwa mmiliki wa kampuni ya Richmond Development (LLC) na kuonyesha kwamba, tuhuma hizo na nyingine hazina ushahidi.
Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa upande mmoja baada ya upande wa Kubenea kutokuhudhuria mahakamani.
Mahakama imetaka waombe radhi ukurasa wa mbele na kutochapisha habari yoyote inayowez akumkashifu mwekezaji huo ambaye Mengi nae amemwita 'Fisadi Papa' nae Rostam akamwita fisadi Nyangumi. Wote ndio walewale au mnabisha??!!!

1 comment:

Anonymous said...

Kuna kampeni ya kupotosha ukweli kuhussu ile ''ajali''.
Kwanza mkuu wa polisi wa Iringa alishasema eti ilikuwa ajali ya kawaida huku akikiri kwamba uchunguzi unaendelea.
Pili blog ya Godwin ilishasema kwamba eti chanzo chja ajali ni shimo katika barabara mbovu ya Mbeya Iringa- lakini katika taarifa yake hiyo alikuwa hajamhoji mbunge wala dereva wake lakini kapata conclusion hivyo tu.Kashimo kenyewe anatuonyesha kalikosababisha ajali kadogo- si kakuagusha cruiser au hata hilux.
Tatu hata Tanzania Daima sasa inageuka na kudai kwamba ilikuwa uzembe wa dereva wa mbunge- wnadai wamezungumza na dereva wa lori ambae alikwenda ofisini kwao.Jana walikuwa wa gazeti la kwanza kutoa taarifa kwamba kulikuwa na lori ilihusika katika hii ajali- magazeti mengine hayakusema hivyo. Comments kwenye blog hii ndiyo ilikuwa taarifa ya kwanza kabisa kusema kulikuwa na lori iliyokimbia ajabu baada ya ajali. Huyu dereva mbona wa ajabu, imetokea ajali hakusimama, taarifa zinamtaja yeye kugonga gari la mbunge alafu haendi polisi anakwenda kwenye gazeti la Tanzania Daima!!!
Mchoro wa ajali wa Polisi kwa Taarifa hauonyesjhi hata picha ya lori!!!Kana kwamba haikuwepo lori kabisa!!!!
Lori ilikuwa na viyoo tinted na kabla tu ya kuigonga gari ya mbunge dereva wa lori aliteremsha kioo na kuiangalia kwa chini gari ya mbunge ilipokuwa ikimalizia kumpita akaibetua gari ya mbunge pembeni kwa nyuma. Patamu hapa ndugu yangu.Kuna kampeni ya kuficha ukweli wa yaliyomsibu mgombea haki wetu mbunge wa Kyela alipogongwa juzi!!!
Kama jasiri ndugu yangu weka maoni haya na utaona kama hukupatwa na virusi.