Thursday, June 25, 2009

BAJAJ


Nimekuwa nashangazwa na maamuzi yanayotolewa katika nchi hii, unakuta kiongozi wa juu anasema hiki baadae anakanusha. Sasa imetokea mpaka kw aviongozi wa kijeshi kama Kamanda wa polisi Mkowa wa Dar es salaam, Suleyman Kova. Katoa amri ya kupiga marufuku Bajaj kuingia mjini mara akasema haziruhusiwi pamoja na pikipiki (Maalufu kama Bodaboda, huko jirani). Huko Bungeni unapelekwa muswada wa kuwezesha vyombo hivyo kutoa huduma kwa wananchi. Sasa ninachojiuliza, nchi hii inatawaliwa bila ya mawasiliano? Ajali za Bajaj zinasababishwa na madereva wake ama madereva wa taxi ambao hawazitaki? Jeshi la polisi linatakiwa kulinda heshima kwani jana Kova kauibuka tena na kasema zinaruhusiwa. Sijui inamaanisha nini? Badala ya wao kufuata chanzo cha ajali zinazotokea mara kwa mara. Kuna watu ambao tumetumia tunajua umuhimu wake. wawaache wajasiliamali wajiinue kiuchumi.

No comments: