Wednesday, June 24, 2009

BUNGE


Wabunge wa wamechacha katika kikao cha Bunge kinachoendelea, kila mmoja analalama, wengine wanashutumu mawaziri kwa kuwabania. wamewasha moto sijui mambo yatakuaje katika mabunge yanayofuata.
Mbunge wa Mchinga, Mudhihil kamshukia ndugu yake wa Mkoa wa Lindi, Bernard Membe kwamba anafanya mtimanyongo ili kiwanda cha Saruji kisijengwe katika jimbo lake. Membe ni wa Mtama hukohuko Lindi.
AkasemaKuna waziri ana hindaskama nyoka wa mdimu, hali ndimu wala majani yake, lakini mtu akitaka kuchuma anambania. Akaongeza kuwa hatamtaja, lakini akasisitiza kuwa Kondoo wa Manyoya atazizima mwenyewe na kujitokeza hadharani.Ana hamu ya urais mwaka 2015.
Jana, Membe kasema kuwa suala hilo linamuhusu yeye kwa hivyo atachukua hatua za kichama chao! Mambo hayo.
Beatrice Shelukindo nae katoa mpya anasema kuna waziri anajipitisha jimbo la Kilindi. Na kusema kuwa watendaji wamekuwa na ugonjwa wa kufanya mambo kama watakavyo na kudai kuwa serikali inaumwa inahitaji mambo ya masheikh na wachungaji!
Mzindakaya nae akaibuka na kusema kuwa wabunge wa CCM watembee kifua mbele kwa kujivunia maendeleo walioletea wananchi. Mbunge huyo ambaye amedumu ndani ya jumba kubwa pengine kuliko asilimia 99 ya wabunge waliopo, alisema kuwa kwa mmiaka yote aliyokuwamo huko,wabunge wa sasa ndio wamefanya kazi zaidi tokea uhuru! Mambo hayo
Sijui tunaelekea wapi, ama Uchaguzi unakaribia?

No comments: