

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Anisseta Wambura aliyaeleza hayo jana mara baada ya Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro, kudai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba tarehe za kuendelea kusikilizwa zilikwishapangwa.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, hakimu Wambura alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machi 8 hadi 9, mwaka huu na kuamuru washtakiwa wote wawepo siku hiyo.
No comments:
Post a Comment