Thursday, August 05, 2010

DR SLAA SONGEA

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willbrod Slaa, jana alipanda jukwaani saa 12.04 na kumaliza saa 12.30 jioni, huku akieleza kuwa kuchelewa kwake kumetokana na Helkopta yake kupata hitilafu akitokea mjini Songea, hali iliyomlazimu kukodi ndege ya dharura ili aweze kuwafikia wananchi hao waliokuwa wakimsubiri tangu saa 9 mchana.

Alisema umasikini wa wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi, Mtwara na Ruvuma unatokana na wakazi hao kuikumbatia CCM, na kwamba ni wajibu wao kupima hali zao za maisha miaka 40 tangu Tanzania ipate uhuru huku CCM kikiwa chama pekee kilichotawala.

“CCM ndiyo iliyowafikisha hapo mlipo, miaka 40 tangu uhuru bado hali ya maisha ya watu wa kusini ni duni, barabara ni moja tu ya lami, ukiacha hiyo utang’atwa na nyoka maporini” alibeza mgombea huyo.

Baadhi ya wasikilizaji wakiongea na mwandishi wa habari hizi walimsifu Dk. Slaa kwa hotuba yake ya ushawishi, huku wengine wakimdhihaki kwa madai kuwa pweza aliyeitabiria Hispania kutwaa kombe la dunia pia amemtabiria Dk. Slaa kuwa rais.

“Dk. Slaa kwangu namuona ni mtu anayekerwa na matatizo ya watanzania maana hata hotuba yake imeweka wazi na kuchambua matatizo yetu……pweza amemtabiria kuwa rais” alisema Joshua George


No comments: