Thursday, August 26, 2010

KAMPENI ZA KIKWETE NGARA


Mkutano wa kampeni kwa mgombea wa CCM uliokuwa ufanyike mjini Ngara jana jioni ulilazimika kuahirishwa baada ya helkopta aliyokuwa akitumia kushindwa kumpeleka mjini humo kutokana na hali mbaya ya hewa.
Hata hivyo ilimlazimu Rais Kikwete kutumia barabara ambapo aliwasiri mjini humo usiku jkwajili ya kuongea na wananchi, hivyo mkutano huo umeahirishwa hadi leo mapema asubuhi.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya posta ya zamani kwa ajili yasikiliza hotuba hiyo, waliambiwana Mwenyekiti wa CCM Hellen Adrian, baadae jana saa 11 jioni kuwa mkutano huo usingekuwepo hadi leo.
Baadae usiku Rais aliwasiri kwas njia ya barabara na kuandaliwa futari na kinamama wa wilayani humo kama inavyoonekana alipopokelewa kwa jili ya masafa zaidi kwajili ya kampeni.

No comments: