Friday, August 27, 2010

MSAADA KWA YATIMA

Osman Kazi akizungumza katika hoteli ya Movernpick Royal Palm leo asubuhi.
Meneja wa Operations wa Movernpick akizungumzia msaada wa hoteli yake.

Baadhi ya walezi wa yatima waliokuwepo katika mkutano huo wakisikkiliza mpango mzima.


Mkurugenzi wa PSET, Osman Kazi akizungumzia bonanza ambalo amaenadaa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya watoto yatima siku ya Idd pili katika viwanja vya leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wataandaliwa michezo na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula na vinywaji.Kushoto kwake ni Bi Mwanaisha Magambo wa New Life Orphanage. Kulia ni Mwakilishi wa Royal Palm Seraphin Lusala.

Kazi ameomba wadau wenye moyo mwema na walio na haja ya kuchangia watoto hao wajitolee kwa vitu mbalimbali vinavyoweza kufanikisha siku hiyo ikiwa ni pamoja na uandaaji ambako vinahitajika vyakula, vinywaji vitamu, vifaa vya michezo na hata fedha ili kufanikisha.

Kikubwa ni watu kujitokeza na kujumuika na watoto hao pamoja na familia zao katika siku ya tukio ili kuifanya iwe ya mafanikio zaidi. Hotel Movenpick Royal Palm imejitolea uku,nbi wa mikutano na vinywaji kwa jili ya maandalizi.

Kwa mawasiliano piga simu namba 0713 477300 ama 0715 732333.

PAMOJA TUNAWEZA, INSHAALLAH!!!

No comments: