Friday, September 03, 2010

UJUMBE WA LEOMtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.

Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..


9 comments:

mpenda said...

Umekosea mjomba. ongeza na sifa nyingine nyingi sana za kumpamba kwa kadri utakavyo.lakini hatufai hata kidogo.Hana jipya zaidi ya kupewa sifa kupitia mgongo wa watu.sio kwamba yeye ni mtakatifu sana kama angekuwa mtakatifu asingekimbi kazi ya kumtumikia mungu matokeo yake amekuwa anahangaika na vimada mara huyu kesho yule(zinaa).Huyu atakemea ukimwi kweli.kulipua mabomu na kuongoza nchi ni vitu viwili tofauti.hata wewe ukiamua kuanza kulipua unaweza.Alikuwa mbunge wa Karatu mbona hasemi alifanya nini la maana kwa wana karatu zaidi ya kelele za bungeni tuu.Anashindwa na zito kabwe angalau jimboni kwake analo la kujivunia.
Mpambe utakavyo lakini kwa mwenye akili timamu hawezi kumpa kura yake.Watakao mpa ni wale wenye chuki,ushabiki bila kutafakari na ajenda zao za siri mioyoni.

Anonymous said...

wacha nipige kelelee maana UMETUTUSI KUWA HATUNA AKILI TIMAMU, SASA MUTAUONA HUO WENDAWAZIMU WETU NA UDUMAVU WETU WA AKILI NA UMBUMBUMBU WETU SIKU YA UCHAGUZI.

Kwanza hamna adabu hata kidogo, wala kwenu hakuna wakubwa, hamkufundwa wala kupelekwa porini kufunzwa adabu na mila za kiafrika.

MNATUTUKANA KISHA TUWAPE KURA?? NYIE HALI HII MATUSI TELE HAMJAPATA JE MKIPATA SI MTATUTEMEA MATE USONI? Pelekeni kukosa kwenu ustaarabu huko huko kwa wenzenu wasojua maana ya ustaarabu. Na yeyote anayeposti kitu kama hiki chenye kuanza kukashifu na kutukana watu kwanza anaonyesha na yeye jinsi upeo wake, utu na ustaarabu wake ulipofikia.

NAOMBA KABLA HAMJAPOSTI VITU VYENU WAULIZENI WATU WAZIMA WAKWAMBIENI MAANA KWANZA INAONEKANA MNAJISEMEA TU WALA HAMJUI IMPACT YA HICHO MNACHOKISEMA!

MWISHO PELEKENI ULIMBUKENI NA UPORI PORI WENU HUKO MBELE YA SAFARI, KAJIFUNZENI KWANZA LUGHA ZA KUONGEA NA KADAMNASI, PAMOJA NA ADABU AU ETIQUETTE ZA KUONGEA NA WATU NDIO MJE KUTUOMBA RIDHAA YA KUTUONGOZA.

MAISHANI MWANGU SIJAWAHI KUONA MTU ANAYEOMBA AKIWA ARROGANT, HII MESSAGE IKO VERY ARROGANT, YALE YOTE MLIYOTAKA KUYASEMA YAMEMEZWA NA HIYO ARROGANCE YENU!

Na ninajua mtajibu kwa matusi lakini ndio yale yale asofunzwa na mamaye, sie ulimwengu ndio shule tutamfunza!

Anonymous said...

Mimi nimesoma paragraph ya kwanza kabisa nimeishiwa hamu ya kusoma eti tuna udumavu wa akili? Sasa nyie mliokuwa hamna udumavu wa akili jichagueni ili mjiongoze wenyewe. Yaani hata sijui huko mbele kumeandikwa nini maana sijasoma kabisa huo ujumbe. Hali hii ndio kwangu mie angalau nimemaliza la saba, je huko vijijini ni nani atakubali kutukanwa na watoto ambao ubwabwa haujawatoka bado?

Mwee ustaarabu kweli kazi! Sasa ndio tunaona nini pumba nini mchele! Mkifika mjini kusoma jichanganyeni na WATU ili wawafunze jinsi ya kuongea na watu!

Anonymous said...

sidhani kama haya maoni ya saidi mpenda na wenzake walioshindwa hata kudiriki kuandika majina yao kuepuka aibu na sini juu ya kile walichokizungumza ni kubwabwa na donge moyoni mwao jamani hakuna asiyejua mwelekeo wa tanzania na maisha ya watanzania ni maisha mbovu kwa kila mtanzania acaheni u-ccm kama mnasomeshwa ama mnaish kwa pesa za kifisadi zinazotokana kw amabepari wa ccm jamani eneough is enough we need change change change na msitake kutulazimisha ccm out!

damija said...

ovyo hoja mlizotoa za kitoto nafikiri mnaubaridi ktk ubongo zenu nakubaliana na mtoa ujumbe kwa asilimia 200 si mia moja ccm chariiiiiiiiiiii hatuwataki watoto wenu wanasoma shule za maana wa kwetu ndiyo hivyo wanatumia vitofari kama madawati no no no please ccm stay in tune

Anonymous said...

Na sisi hatuwachagui kwa matusi yenu. Sasa hiyo siku ya uchaguzi ndio mtaona huo "ubaridi katika bongo zetu" Mtayavuna hayo matusi yenu.

Ukiona watu wanakimbilia kutukana hata watu wasiowajua ujue kuwa hata wazazi waliowazaa hawawaheshimu na ni dalili ya kukosa malezi bora yenye maadili na mwisho ni DALILI YA KUISHIWA HOJA NA KUSHINDWA!

Pelekeni matusi yenu Bandarini!

Anonymous said...

CHAMA CHA MATUSI MPOOO! MAJITAKA! lol! Majitaka kweli kweli, kapigeni mswaki kwanza kabla ya kuongea na watu!

Na hampati kitu ng'o mtaambulia Wabunge 10, wanawatosha!

Anonymous said...

Hata we Damija watoto wako wanatumia vitofari? Usiwazuge wenzio nyie mnaotoka chuo cha Sanaa tunajua mko kazini siku zote kwa hiyo usitake kutumia thermometer hapa!

Anonymous said...

Hata Augustino Mrema alitaja mafisadi pale Mwembe yanga mwaka 1996. Je naye ni kiongozi mzuri?