Friday, October 01, 2010

NIMEIPENDA


NILIKWISHA kusema katika safu hii kwamba kipindi cha uchaguzi ni msimu wa vituko na vitimbwi, na kwamba watu wenye akili timamu wanaweza wakaziweka akili zao kando ili washiriki vyema katika shughuli za uchaguzi, kisha wazirejee akili zao na waendelee na shughuli zao za kila siku.

Hawa ni wengi, na tumewaona, tumewasikia na tutaendelea kuwaona na kuwasikia hadi mwishoni mwa Oktoba. Baada ya Oktoba watarudia hali zao za kawaida, na ukiwaangalia wakati huo hutoweza kuamini kwamba ndio wale wale uliowaona na kuwasikia mwezi Septemba.

Mhariri wa gazeti la kila siku Daily News naye kajiunga na kundi hilo kubwa, labda kwa sababu anachelea kuachwa nyuma katika mashindano ya kuweka akili kando kwa muda kama vile kuna manufaa fulani katika kufanya hivyo.

Mhariri huyo, inaelekea, alikerwa sana na taarifa iliyotoka katika gazeti moja linalotoka kila Jumanne (hakulitaja, na kwa siku yake ya kutoka si Raia Mwema!) iliyoarifu kwamba kura ya maoni iliyofanyika kupitia mtandao fulani iliashiria kwamba mgombea urais kupitia CHADEMA anakubalika kwa wale walioshiriki katika kutoa maoni hayo katika mtandao huo. Soma Zaidi...

No comments: