Wednesday, December 29, 2010

CHENGE AKWEPA JELA

Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kindondoni imemkuta na hatia Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi ambaye alikuwa waziri wa Miundombinu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya laki saba kwa kuendesha gari na kuua.

Hata hivyo Chenge alijiondolea adhabu hiyo ya kukaa lupango kwa miaka mitatu na kuamua kulipa faini kwa hiyo sasa yuko huru.

Hukumu hiyo ilitolewa na Kwey Lusema wa mahakama hiyo Habari kamili Baadae.

March 31 2009, huyo alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.

Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa mawili ni ya kusababisha vifo vya watu wawili, na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.


1 comment:

Anonymous said...

chenge umeua na kulipa laki tano unachekelea? utakapokufa utaonana na mungu na atakusomea hukumu ya haki na wala sio ya hawa wanafiki wa kitanzania, kumbuka ditopile...