Thursday, January 06, 2011

NYARANDU AJIONEA KARIAKOO

Waziri wa Viwanda na Bishara, Lazaro Nyalandu akikatisha katika mitaa ya Kariakoo leo kujionea bishara zinavyoendeshwa hasa na 'wamachinga' wa kichuina na wa nchi za jirani. Pembeni yake ni Meya wa Ilala, Jerry Slaaa.
Naibu waziri na Meya walipata taarifa za moja kwa moja kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara.
Wafanyabaishara nao hawakukosa la kusema.
Wengine walilaumu wateja kuishia juu na kubaki na bidhaa kibao.
Kuan wengine walikuwa na jazba kama wanataka kupiga mtu.
Walipopata majibu kutoka serikalini walishangilia na kuonyesha kufurahishwa.
Wengine waling'aka kama wanataka roho ya mtu!
Cheki kama huyu, alitaka kieleweke.

Wenye mabango waliyaweka ili kufikisha ujumbe.
Wengine walionyesha bidhaa zao kwa waziri.

Lakini hali ya chini ya soko ilikuw angumu msongamano na joto la kutisha baadhi ya sehemu feni hakuna.

================================================

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu leo alifanya ziara ya soko la Kariakoo ambako alilakiwa na wafanyabiashara waliokuwa na lawama kibao kuhusu huduma sokoni hapo.

Aidha alitangaza msimamo wa serikali juu ya 'wamachinga' wa nchi za nje ambao aliwataka waondoke nchini katika siku 30 ama wafuate sheria na taratibu za uwekezaji nchini.

Alisema serikali inafanya mapango wa kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanafanya biashara kwa mpangilio na kupachangia pato la taifa na hivyo kuwataka watanzania waache kununua biashara za mikononi.

Hata hivyo wafanyabishara wa Kariakoo shimoni walilalamikia hali ya joto katika soko hilo na Nyalandua aliamuru feni ziongezwe ili kuwe na hewa ya kutosha ndani ya soko hilo anmbalo kwa sasa linashuka umaarufu.

Pia wafanyabishara walitaka serikali iweke mfumo maalum wa masoko jijini ili kuwe na masoko ya Jumla na rejareja ili nao waweze kupata wateja tofauti na sasa ambapo masoko yamekuwa yakifunguliwa kiholela.

1 comment:

Anonymous said...

mbona hujatoa picha hata moja ya mchina anayefanya hizo biashara au wewe ni mwanasiasa sio mwanahabari?