Wednesday, March 09, 2011

DAWA YA LOLIONDO SHWARI!!!!!

Wananchi wakifurika kupata kikombe cha dawa ya Mzee wa Kinyakyusa aishie Loliondo, Mchungaji Ambilikile Mwasapile!
Dawa ikiwa jikoni tayari kwa mgao, kasufuria kadogo katatosha wote?
Tokea mwanzo wa dunia hakujawahi kuwa na Traffic jam kama hii bush!!
Wananchi wakisubiria kumiminiwa dawa ya Uzima na Babu.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limesema linatambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu, Maaskofu wa kanisa hilo Thomas Laizer wa Dayosisi ya Mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.

Askafu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na Kanisa halina mgogoro naye.No comments: