Thursday, January 13, 2011

MAZISHI YA WAPIGANIA HAKI






CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi.

Polisi pekee waliooekana ni wale tu wa usalama barabarani. Barabara kadhaa za jiji la Arusha zilifungwa, na maelfu ya wananchi walitanda kando ya barabara hizo, kushuhudia msafara wa miili ya marehemu ikitoka chumba cha maiti kuelekea viwanja vya NMC, na baadaye kuelekea eneo la mazishi, USA River alikozikwa Ismaili Omar. Mmoja wa marehemu hao, Denis Michael, atazikwa leo Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Mashujaa hao waliuawa na polisi waliokuwa wanapambana na wafuasi na viongozi wa CHADEMA katika kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika viwanja vya NMC, Januari 5, mwaka huu, kudai marudio ya uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha na naibu wake.

Zizi la Arusha lilizizima kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa kishindo katika ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu hao.

Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya. Soma zaidi

1 comment:

Anonymous said...

Naanza kwa kuwasalimu wadau wote na mzee wa sumo,ndugu zangu chadema nafurahishwa na maendeleo yenu mliyofikia mpk hv ss na mmetuonyesha mwanga wa democracy unavyozidi kumulika ktk nchi yetu ya tanzania na kwa kulitambua hilo ni haki yenu kudai kurudiwa kwa uchaguzi wa meya na makamu wake hapo arusha ili haki itendeke.CCM wamekua wakijiamini sn ktk kila jambo na kujiakikishia kwamba watashinda kwenye nyazifa mbalimbali lkn hii ya arusha imezidi.Kwa kuwa walishindwa kiti cha ubunge basi walijua fika na umeya watashindwa ndipo walipojiandaa kufanya dhuluma na ubabe ili mgombea wao awe meya.Hivyo basi kwa kutumia misingi na katiba yenu chadema mnapaswa kuomba kurudiwa kwa uchuguzi huo wa meya wa arusha kwa hekima na busara ili muweze kuuonyesha ulimwengu kuwa matokeo ya awali yalikua si ya halali na naamini kuwa kama mtafuata utaratibu mzuri basi hata mahakama ya kimataifa itaweza kuwasaidia kwa hili na mtashinda kwa kishindo kikubwa sn bila manung'uniko.Lakini mkisema muandamane kwa kuishinikiza na kuilazimisha serikali uchaguzi huo urudiwe,watazidi kuwapiga na kuwaua km walivyofanya kwa CUF nakutojali lolote sababu tu wao ni watawala wa nchi na maamuzi yao yapo mikononi mwao hivyo nawasii sn chadema mtumie njia nyingine na sio maandamano natumaini mungu atawaongoza mtachukua kiti cha meya wa arusha.Mdau kutoka Dubai muri na email yangu ni mugo.muriuki@yahoo.com